China imesitisha mazungumzo ya kudhibiti silaha na Marekani
18 Julai 2024Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lin Jian amesema kitendo cha hivi karibuni cha Marekani kurudia kuiuzia Taiwan silaha kunahatarisha mazingira ya kisiasa kwa ajili ya kuendelea na mashauriano ya kudhibiti silaha.
Lin alisema China iko tayari kudumisha mawasiliano katika udhibiti wa silaha za kimataifa, lakini Marekani lazima iheshimu misingi ya China na kujenga mazingira muhimu kwa ajili ya majadiliano.
Maafisa wa Marekani na China walianzisha tena majadiliano kuhusu silaha za nyuklia mwezi Novemba, lakini mazungumzo rasmi ya kudhibiti silaha hayakutarajiwa kufanyika hivi karibuni katikati ya wasiwasi wa Marekani kuhusu China kuharakisha katika kutengeneza silaha za nyuklia.
China inadai kisiwa hicho chenye mamlaka yake ya kidemokrasia ni himaya yake.