1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China ina wasiwasi kuhusu mvutano katika rasi ya Korea

31 Oktoba 2024

China imesema inawasiwasi kuhusu hali katika Rasi ya Korea, baada ya Korea Kaskazini kusema imefanya majaribio ya moja ya makombora yake yenye nguvu zaidi.

China ina wasiwasi kuhusu mvutano katika rasi ya Korea
China ina wasiwasi kuhusu mvutano katika rasi ya KoreaPicha: JUNG YEON-JE/AFP

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo Lin Jian, amesema wameona ripoti husika na kwamba kama taifa jirani la rasi hiyo, linafuatilia hali inavyoendelea katika eneo hilo.

''Tunaamini kwamba kudumisha amani na utulivu kwenye rasi hiyo na kuunga mkono suluhisho la kisiasa kuhusu suala la rasi hiyo ni kwa maslahi ya pamoja ya pande zote, na tuna matumaini pande zote zitashirikiana kulifanikisha hilo.'', alisema Jian.

Jaribio hilo la kombora linafanyika saa chache baada ya wakuu wa ulinzi wa Marekani na Korea Kusini kuitaka Korea Kaskazini kuondoa wanajeshi wake kutoka Urusi, na kuonya kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini waliovalia sare za Urusi wako nchini humo kwa uwezekano wa kutumika katika vita nchini Ukraine.