1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaendelea na luteka za kijeshi kuzunguka Taiwan

9 Aprili 2023

China inaendelea na mazoezi ya kijeshi kuzunguka kisiwa cha Taiwan kwa siku ya pili kwa kile inachoita onyo kali kwa kisiwa hicho kinachojitawala baada ya rais wa kisiwa hicho kukutana na Spika wa bunge la Marekani.

Chinesische Militärübungen vor Taiwan
Picha: Thomas Peter/Reuters

China inaendelea na mazoezi ya kijeshi kuzunguka kisiwa cha Taiwan kwa siku ya pili kwa kile inachoita onyo kali kwa kisiwa hicho kinachojitawala baada ya rais wa kisiwa hicho kukutana na Spika wa bunge la Marekani. Ziara ya nchini Marekani iliyofanywa na Rais wa Taiwan Tsai Ing-Wen imeikasirisha China. Katika mazoezi hayo yaliyoanza Jumamosi, China imepeleka manowari, ndege za kivita na makombora kwenye bahari ya kuzunguka Taiwan kwa lengo la kutoa onyo kali. Wizara ya ulinzi wa Taiwan imesema manowari tisa zinashiriki katika luteka hiyo. Katika kadhia nyingine, mnamo wiki hii China imetangaza kuweka vikwazo dhidi ya mwakilishi wa Taiwan kwenye Umoja  wa Mataifa na dhidi ya mashirika mawili ya Marekani. China imesema itampiga marufuku balozi wa Taiwan nchini Marekani kuingia China na imemlaumu balozi huyo kwa kusababisha mvutano.