1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China inakutana na Umoja wa Ulaya kwa majadiliano

7 Desemba 2023

Wawakilishi kutoka Beijing na Brussels wanakutana hii leo kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na China katika mji mkuu wa China, Beijing baada ya miezi kadhaa ya mivutano ya kibiashara baina yao

EU-China-Dialog zu Sicherheitsfragen
Picha: Pedro Pardo/AFP

Marais wa Baraza la Ulaya Charles Michel Ursula von der Leyen wa Halmashauri Kuu ya Ulaya wanatarajiwa kurejesha utulivu wa kibiashara na siasa za maeneo hayo watakapokutana na Rais wa China Xi Jinping na maafisa wengine wa serikali.Brussels inaamini kwamba makampuni ya Ulaya hayana fursa ya kutosha katika soko la China.Kabla ya kuondoka, von der Leyen aliionya China dhidi ya mienendo yake isiyo sawa ya kibiashara, akiangazia pamoja na masuala mengine, ugumu kwa makampuni ya Ulaya kuyafikia masoko ya China. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW