1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China, Japan zadhamiria kuimarisha uhusiano

11 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, amesema anatazamia nchi yake na Japan zitapata muafaka wa kuyarejesha mahusiano yao kwenye njia sahihi.

Waziri Mkuu wa China, Li Qiang.
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang.Picha: Pedro Pardo/AFP

Japan na China zimekuwa zikijaribu mataifa hayo mawili yakijaribu kulainisha misimamo yao mikali kwenye uhasama wao wa muda mrefu.

Akizungumza na mwenzake wa Japan, Shigeru Ishiba, kandoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini na Mashariki mwa Asia (ASEAN) mjini Vientiane nchini Laos, Li alisema matarajio yake ni kuwa nchi hizo mbili zinaweza kuendelea kujadiliana na kushirikiana kwa maslahi ya utulivu, maendeleo ya viwanda na mfumo huru wa biashara.

Soma zaidi: Japan yalalamikia 'harakati za jeshi' China

Kwa upande wake, Ishiba alisema Japan iko tayari kushirikiana na China na kutatuwa vikwazo vilivyopo kwenye ngazi za zote.

Mazungumzo ya mawaziri hao wakuu yamefanyika siku moja tu baada ya hapo jana mawaziri wao wa mambo ya kigeni kupigiana simu.