1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China: Kigogo ajaye wa nyumba juu ya kamba

16 Agosti 2023

Kampuni kubwa zaidi ya ujenzi wa nyumba nchini China, Country Garden inapambana kuepuka kuwa muflis. Uwezekano wa kufilisika unaweza kusababisha matatizo kwa bei za nyumba na uchumi mpana.

China, Beijing  | Eneo la ujenzi la Country Garden
Country Garden iliahidi "maisha ya nyota tano" kwa wananchi.Picha: Ichiro Ohara/Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Watunga sera wa China wanakabiliwa na wito wa kufanya zaidi kusaidia soko la nyumba linalodorora baada ya msanidi mkubwa zaidi wa majengo, Country Garden, kuonya kuhusu hasara ya mabilioni ya dola na kukosa malipo ya dhamana.

Kampuni hiyo ya 138 kwa ukubwa duniani, kulingana na jarida la biashara la Fortune, ilionya wiki iliyopita kwamba kutokana na "kupungua kwa mauzo katika sekta ya nyumba," ilikuwa karibu kupoteza kati ya dola bilioni 6 na 7 katika kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni 2023.

Shanghai yakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya Corona

Hadi hivi karibuni, Country Garden ilionekana kuokolewa kutokana na mdororo wa sekta ya nyumba ulioikumba China wakati wa janga la UVIKO-19 wakati serikali ya Rais Xi Jinping ilipoweka kikomo juu ya kiasi gani wajenzi wa nyumba wanaweza kuchukua.

Katika miongo miwili iliyopita, kadiriwatu wa China walivyozidi kuwa tajiri, ongezeko kubwa la ujenzi ambalo halijawahi kutokea lilisababisha kuongezeka kwa bei ya nyumba mara nne. Mamia ya mamilioni ya watu waliweka karata ya kuwekeza akiba zao kwenye sekta ya nyumba ambako walidhani zingekuwa salama zaidikuliko soko la hisa la nchi hiyo lisilotabirika.

Kwanza Evergrand, sasa Country Garden

Lakini baada ya miaka ya ukuaji wa juu, udhibiti mpya wa deni la serikali ulisababisha mauzo ya nyumba na bei kushuka, na kuiathiri vibaya hasa kampuni moja ya nyumba ya China Evergrande.

Kampuni hiyo ya pili kwa ukubwa ya ujenzi nchini China, Evergrande ilikuwa imezoea kutumia amana za wawekezaji kwenye miradi ya siku zijazo kufadhili ujenzi wa sasa. Mnamo 2021, Evergrande ilitangaza kuwa ina deni la dola bilioni 300 na baadaye ikakosa kulipa sehemu ya deni lake, pamoja na wenzake wengi.

Ukosefu wa ajira kwa vijana unaongezeka nchini China baada ya soko la nyumba kuporomoka na kusababisha kushuka kwa ukuaji wa uchumi.Picha: Xiang Yang/picture-alliance/dpa

"Wakati mgogoro wa China Evergrande ulipotokea, watu waliogopa kwamba mengine yangefuata, lakini bila shaka sio Country Garden. Ilikuwa na manufaa kidogo kuliko Evergrande," Alicia Garcia-Herrero, mwanauchumi mkuu wa Asia Pacific katika benki ya uwekezaji ya Ufaransa NATIXIS, aliiambia DW.

China: Marekani yakiuka kanuni za uchumi wa soko na sheria

"Bila onngezeko endelevu la bei, muundo mzima wa sekta ya nyumba hauwezi kuedelea na hata kampuni kama Country Garden haiwezi kumudu," Garcia-Herrero mwenye makao yake Hong Kong aliongeza.

Uvumi kuhusu matatizo ya Country Garden umekuwa ukiongezeka kwa miezi kadhaa. Hisa zake zimeshuka kwa zaidi ya asilimia 75 tangu Januari. Siku ya Jumatano, hisa za Country Garden zilikuwa zikiuzwa kwa dola za Hong Kong 0.83 (€0.093, $0.10).

Kampuni ya amana yakosa malipo

Katika kuongeza chumvi kwenye kidonda, kampuni kubwa katika sekta ya dhamana ya China yenye thamani ya dola trilioni 2.9, Zhongrong International Trust, ilikiri wiki hii kuwa imekosa malipo kadhaa ya bidhaa za uwekezaji, na kufanya uingiliaji kati wa serikali kuwa na uwezekano mkubwa zaidi.

Kampuni za dhamana ni sehemu muhimu ya mfumo wa benki kivuli wa China kwani hukusanya akiba za kaya ili kuwekeza katika nyumba, hisa na bidhaa. Wanaelekea kuwa na mfiduo wa nje wa sekta ya mali ya nchi.

Kenya: Kufurika kwa wafanyibiashara kutoka China

Wakiwa tayari wametoa msaada kwa waendelzaji na vivutio kwa wanunuzi na waboreshaji wa nyumba kwa mara ya kwanza, viongozi wa China "wana uwezekano mkubwa" wa kuinusuru Country Garden, Pushan Dutt, profesa wa uchumi katika shule ya biashara ya Insead nchini Singapore, aliiambia DW.

"China imepambana na tatizo la ukuaji usio na usawa unaotokana na uwekezaji huku sekta ya nyumba ikiongoza kwa zaidi ya muongo mmoja," Dutt alisema. "Kila wakati wanajaribu kushughulikia suala hili, ukuaji unapungua, na wanarudi kwenye suluhisho sawa la uokoaji, kusukuma ukwasi, na kupunguza viwango vya riba."

Kufilisika kutakuwa na athari mbaya

Kwa vile sekta ya nyumba ya China inachangia kiasi cha asilimia 30 ya pato la taifa (GDP), kuanguka kokote kwa Country Garden kunaweza kuwa na athari kwenye mfumo mzima wa kifedha.

Ufufukaji wa China baada ya UVIKO -19 tayari ni dhaifu zaidi kuliko ilivyotarajiwa kutokana na kupungua kwa mahitaji ya kimataifa ya mauzo ya nje ya China na ukosefu wa mahitaji ya ndani.

Country Garden iliuza karibu theluthi mbili ya nyumba mwaka jana katika miji midogo ya China.Picha: Sheldon Cooper/SOPA Images/ZUMA/picture alliance

Kurudi nyuma kumekuwa dhaifu sana, wachumi kadhaa mwezi uliopita walishusha utabiri wa Pato la Taifa kwa mwaka hadi asilimia 5 kutoka asilimia 5.5. Beijing ilisema wiki hii itaacha kuchapisha takwimu za ukosefu wa ajira kwa vijana kwani ziko juu sana.

Profesa wa Insead Dutt alionya juu ya hatari ya kuambukizwa kutokana na kutokuza soko la nyumba, akibainisha kuwa China inaweza kukabiliwa na "miaka ya ukuaji duni" ambayo Japan ilikabiliana nayo mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Alikuwa akimaanisha kile kinachojulikana kama muongo uliopotea wa Japani kufuatia kupanda kwa soko la mnyumba ambako kulisababisha nyumba ya wastani ya Tokyo ikifikia mara 15 ya wastani wa mshahara wa mwaka hadi ilipopaanguka.

"Kuzuwia athari zitokanazo na mtikisiko wa sekta ya nyumba kutahitaji kichocheo kikubwa zaidi cha fedha kuliko kiwango mamlaka ziko tayari kutoa hadi sasa," Gerwin Bell, mwanauchumi mkuu wa kampuni ya PGIM ya Asia, aliliambia shirika la habari la Reuters wiki hii. "Tunatarajia mamlaka ya China hivi karibuni kufikia hitimisho sawa."

Wengine, hata hivyo, hawana imani na uingiliaji kati wa moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na Maggie Hu, profesa msaidizi wa masuala ya nyumba na fedha katika Chuo Kikuu cha China cha Hong Kong, ambaye aliiambia DW uwezekano wa uokoaji wa Country Garden ulikuwa "chini kabisa."

"Ikiwa itageuka kuwa dharura, sera zitatekelezwa kulinda ujenzi wa mali zilizouzwa kabla, kuhakikisha ustawi wa wanunuzi wa nyumba na benki zinazohusika," Hu aliiambia DW.

Wachina wako tayari kwa mporomoko wa kudumu ya sekta ya nyumba

Haijalishi ikiwa watunga sera wataingilia kati na jinsi gani, wanauchumi wengi wanatarajia anguko la sekta ya nyumba kuendelea, hasa nje ya miji mikubwa ya Beijing na Shanghai.

Jengo la kampuni ya Evergrande lililoko mjini Shanghai. Kampuni hii ndiyo ilianza kufilisika na sasa Country Garden inakabiliwa na kitisho sawa.Picha: Xing Yun/Costfoto /Xing Yun/picture alliance

Wastani wa bei mpya za nyumba katika miji midogo 35 iliyochunguzwa na Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ilishuka kwa mwezi wa 17 mfululizo mnamo Juni mwaka baada ya mwaka.

"Madhara mabaya [ya ajali] yatajulikana hasa katika miji ya daraja la pili au la tatu," Hu alitabiri. "Hasa miji hiyo inakabiliwa na uchumi unaopungua na idadi ya watu wanaozeeka na idadi kubwa ya watu."

Beijing ina nia ya kuzuia msongamano wa nyumba ambazo hazijakamilika, hasa katika miji midogo, ambapo Country Garden imekuwa ikifanya kazi zaidi katika ujenzi na ina wastani wa nyumba milioni zisizokamilika.

Wakati kampuni hiyo iliahidi watu wengi fursa ya kupata "maisha ya nyota tano," wengi wako karibu kutazama ndoto zao zikiyeyuka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW