1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China kuimarisha uhusiano wake na Korea Kaskazini

12 Septemba 2023

China imesema leo kuwa inanuia kuimarisha ushirikiano na Korea Kaskazini katika "fani mbalimbali" wakati Kim Jong Un akiwasili Urusi katika ziara yake nje ya nchi baada ya miaka minne.

Msemaji wa wozara ya Mambo ya Nje China Mao Ning
Msemaji wa wozara ya Mambo ya Nje China Mao NingPicha: Kyodo/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Mao Ning ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa uhusiano wa China na Korea Kaskazini unaendelea vizuri.

Shirika la habari la serikali la Urusi Ria Novosti limeripoti kuwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewasili nchini humo leo.

Soma pia:Biden azungumza na Waziri mkuu wa China

Kulingana na msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, kiongozi huyo wa Korea Kaskazini anatarajiwa kukutana na Rais Vladimir Putin baadaye wiki hii.

Ziara hiyo ni kwanza kwa Kim kuifanya nje ya nchi tangu janga la UVIKO-19.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW