1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China kurejesha amani kwa Wapalestina kupitia UN

6 Novemba 2023

China yaahidi kurudisha amani maeneo ya wapalestina katika nafasi yake ya mwenyekiti wa baraza la usalama.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

China imesema itafanya kadri ya uwezo wake kurudisha amani katika maeneo ya Wapalestina wakati ikitwaa uwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Hayo yameelezwa na wizara yake ya mambo ya nje leo Jumatatu katika wakati ambapo mivutano imeongezeka katika eneo la mashariki ya Kati.

Soma pia:China na Urusi waikosoa Marekani katika mkutano wa kijeshi

Msemaji wa wizara hiyo Wang Wenbing amewaambia waandishi habari kwamba China itafanya kila iwezalo katika uwezo wake kuwashawishi wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutimiza wajibu wao, kufanya majukumu yao na kujenga maridhiano,pamoja na kuchukua hatua zinazistahiki, haraka iwezekanavyo kutuliza mgogoro wa hivi sasa na kulinda usalama wa raia,ili kurudisha amani.

Taarifa ya China imekuja wakati Israel ikizidisha opreösheni yake ya kijesho dhidi ya kundi la Hamas.

China ilitwaa uwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita,nafasi ambayo ni ya kupokezana.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW