1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China: Marekani iwe makini na matendo yake

15 Septemba 2025

China imetoa onyo kwa Marekani baada ya Rais Donald Trump kuzitaka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Kujihami NATO kutoza ushuru mkubwa kwa bidhaa za China na kuacha pia kununua mafuta ya Urusi.

China | Lin Jian
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China, Lin JianPicha: Ichiro Ohara/Yomiuri Shimbun/AP Photo/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China, Lin Jian, amesema matakwa ya China yakiathirika kwa namna yoyote  ile, itachukua hatua sawa kulinda usalama na maslahi yake. Jian amesema tabia ya Marekani ni ya unyanyasaji.

Hata hivyo, wizara ya uchumi ya China ilisema katika taarifa tofauti kwamba inatumai Marekani itakuwa makini katika maneno na matendo yake na kutatua tofauti zake za kibiashara na kiuchumi kupitia mazungumzo.

Awali Trump alivihusisha vikwazo zaidi vya Marekani dhidi ya Urusi kwa mataifa ya NATO akiweka ongezeko la ushuru la asilimia 50 hadi 100 kwa bidhaa za China na kukataa mataifa hayo kununua mafuta ya Urusi. Trump alisema anaamini hatua hiyo itasaidia kuvimaliza vita vya Urusi na Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW