China na Brazil zaonya dhidi ya matumizi ya nyuklia Ukraine
28 Septemba 2024Matangazo
Kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa katika Umoja wa Mataifa ambayo pia ilitiwa saini na Afrika Kusini na Uturuki, mataifa hayo yametoa wito wa kujiepusha na matumizi au kitisho cha silaha za maangamizi makubwa, hususan silaha za nyuklia na za kibayalojia.
Mataifa hayo yanayoendelea kiuchumi yamesisitiza umuhimu wa suluhisho la amani kwa migogoro yote ya kimataifa.
Wiki hii Rais Putin alitishia kutumia silaha za nyuklia iwapo kutatokea shambulio kubwa katika ardhi ya Urusi. Huku Ukraine ikitaka kupewa silaha zaidi kutoka nchi za Magharibi ili kufanya mashambulizi katika ardhi ya Urusi.
Mataifa mengine yaliojiunga na wito huo wa Brazil na China ni pamoja na Algeria, Bolivia, Colombia, Misri, Indonesia, Kazakhstan, Kenya na Zambia.