1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Japan zakamilisha mazungumzo ya biashara na uchumi

2 Desemba 2007

Beijing:

China na Japan zimekamilisha mazungumzo ya siku mbili ya ngazi ya juu ya kibiashara na kiuchumi mjini Beijing.

Katika taarifa ya pamoja pande hizo mbili zimeahidi miongoni mwa mengine kuimarisha juhudi za kuunda eneo la biashara huria la eneo lao, na kukuza hali ya kujitosheleza kwa nishati.

Hata hivyo zilishindwa kuutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu haki ya utafiti wa gesi katika bahari ya mashariki mwa China. China ilianza uchimbaji katika eneo hilo miaka minne iliopita.