SiasaChina
China na Marekani wakubaliana kuandaa mkutano wa Xi na Biden
28 Oktoba 2023![Mawaziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na Anthony Blinken (kulia) wa Marekani walipokutana kwa mazungumzo mjini Washington, Oktoba 26,2023](https://static.dw.com/image/67228502_800.webp)
Matangazo
Maafisa hao hata hivyo walipozungumza na waandishi wa habari hawakufafanua zaidi ikiwa mkutano huo utafanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa kiuchumi kwa Mataifa ya Asia na Pasifiki, APEC mwezi ujao huko San Francisco.
Matamshi haya yanatolewa baada y mazungumzo yaliyodumu kwa masaa kadhaa kati ya waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na maafisa hao mjini Washington.
Wang Yi, waziri wa kwanza wa mambo ya nje wa China kuzuru Marekani tangu mwaka 2018, alikutana kwanza na rais Biden, waziri wa mambo ya nje Anthony Blinken pamoja na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa White House, Jake Sullivan.