1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

China yahimiza mazungumzo kumaliza msuguano na Marekani

27 Oktoba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema China na Marekani wana tofauti zinazohitaji mazungumzi ya kina na mapana ili kupunguza misuguano na kuimarisha mahusiano baina ya mataifa hayo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na wa Marekani Anthony Blinken wakipeana mikono wakati Wang alipizuru Washington Oktoba 26, 2023
Mawaziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na wa Marekani Anthony Blinken wakipeana mikono wakati Wang alipizuru Washington Oktoba 26, 2023Picha: Jose Luis Magana/AP/picture alliance

Waziri Wang Yi amesema hayo alipoanza ziara yake mjini Washington jana Alhamisi.

Wang akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken kwamba mataifa hayo mawili yana maslahi muhimu na changamoto zinazofanana ambazo zinahitaji kusuluhishwa kwa pamoja.

Blinken alijibu kwa kusema tu kwamba anakubaliana na Wang.

Hii ni ziara ya karibuni katika msururu wa hatua za kidiplomasia kati ya mahasimu hao wawili wa kimkakati wanaosaka kusuluhisha tofauti na maandalizi ya mkutano wa kilele unaotarajiwa kati ya rais Joe Biden na Xi Jinping wa China.