1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China na Ufilipino zafikia makubaliano kuhusu eneo la bahari

22 Julai 2024

China na Ufilipino zimetangaza makubaliano ya kukomesha mzozo kuhusu eneo la bahari ya Kusini mwa China. Nchi hizo mbili zinadai umiliki wa eneo la bahari la Ayungin, ambalo linadhibitiwa na Manila.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Tingshu Wang/REUTERS

Ufilipino ilipeleka meli ya kivita katika eneo hilo mnamo mwaka wa 1999 ili kuongeza nguvu madai yake. Kundi dogo la wanajeshi wa Ufilipino limepelekwa katika eneo hilo la bahari.

Lakinijeshi la wanamaji la Ufilipino limekabiliana mara kadhaa na meli za ulinzi wa pwani za China wakati zikijaribu kupeleka vifaa na biadhaa na kuwabadilisha mabaharia. 

Soma pia:Ufilipino na China zafikia makubaliano kuzima mgogoro

Meli za China zilitumia mizinga ya maji na kuzizuia meli za Ufilipino kufika katika kituo hicho. Sasa, Beijing na Malina zimesema zimefikia maelewano kuhusu suala hilo. Hata hivyo hazikutoa maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo.

China inahusika na mizozo kama hiyo na majirani zake, wakiwemo Brunei, Malaysia, Taiwan na Vietnam. Makabiliano katika Bahari ya Kusini mwa China aghalabu yamechochea hofu ya kuzuka mgogoro mkubwa wa kikanda. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW