China, Ujerumani kuzingatia uwazi na ushindani wa haki
25 Februari 2026
Matangazo
Hayo ni kulingana na kauli ya pamoja iliyotolewa na Rais wa China Xi JinPing pamoja na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz aliye ziarani Beijing.
Kando ya hayo mataifa hayo yamesema yanaunga mkono juhudi za kupata makubaliano ya kusitisha vita na amani ya kudumu nchini Ukraine kwa kuzingatia mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Mabadiliko ya tabia nchi kuzingatiwa
China na Ujerumani zimekubaliana pia kuendeleza mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Katika hatua nyingine baada na mazungumzo yake na Rais Xi, Kansela wa Ujerumani amesema China itanunua takriban ndege 120 kutoka kwa kampuni kubwa ya usafiri wa anga ya Ulaya ya Airbus.