1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China, Urusi zafanya doria pamoja Bahari ya Pasifiki

Angela Mdungu
14 Julai 2024

Majeshi ya wanamaji ya China na Urusi, yameendesha zoezi la pamoja la doria magharibi na kaskazini mwa bahari ya Pasifiki

Meli za kijeshi za China na Urusi zikiwa zimetia nanga baada ya mazoezi ya kijeshi Julai 24, 2023
Urusi na China zimfanya pamoja doria katika Bahari ya PasifikiPicha: Yuri Smityuk/TASS/picture alliance

Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumapili 14.07.2024 na  televisheni ya taifa ya China CCTV, zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa pamoja wa kila mwaka kati ya mataifa hayo hayo mawili.

Soma zaidi: Urusi na China zafanya luteka za pamoja za kijeshi

Taarifa hiyo hata hivyo imebainisha kuwa, mpango huo hauilengi nchi nyingine yoyote. Imeongeza pia kuwa, hatua iliyochukuliwa na China na Urusi, haihusiani kwa namna yoyote na hali ya sasa ya kimataifa na kikanda. Hii ni mara ya nne kwa nchi hizo mbili kufanya doria ya pamoja katika eneo hilo la bahari.

China na Urusi zimeimarisha mahusiano yao ya kiuchumi na kijeshi, jambo linalozusha hofu na mashaka kwa mataifa ya Magharibi ambayo yanalenga kukabiliana na ushawishi unaoongezeka wa China.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW