SiasaAsia
China, Ufilipino zagongana Bahari ya Kusini
22 Oktoba 2023![Meli za China na Ufilipino kwenye makabiliano katika Bahari ya Kusini mwa China siku ya Jumapili (Oktoba 22).](https://static.dw.com/image/67177091_800.webp)
Matangazo
Kukabiliana kwa wanajeshi wa majini wa pande hizo mbili siku ya Jumapili (Oktoba 22) ni mvutano wa hivi karibuni zaidi katika msururu wa mivutano katika bahari hiyo.
Mataifa hayo yamekuwa yakizozania udhibiti wa maeneo ya Bahari ya Kusini mwa China na hasa katika eneo la Thomas Shoal ambalo ni sehemu ya visiwa vya Spratly.
Ufilipino ilikuwa ikiwapelekea vifaa wanajeshi wake walioko katika meli ya zamani iliyotumiwa katika Vita vya Pili vya Dunia, hatua iliyoilazimu China kuingilia kati na kuzuwiya operesheni hiyo.