China yaamuru kufungwa ubalozi mdogo wa Marekani Chengdu
24 Julai 2020Hali ya wasi wasi imefikia kiwango kipya cha juu katika kile wakati wote kilichokuwa barabara iliyojaa mashimo na mawe, wakati matarajio na dhamira ya taifa hilo linaloinukia kuwa taifa kubwa yakikinzana na yale ya taifa ambalo tayari ni taifa lenye nguvu kama Marekani.
China imeamuru kufungwa kwa ubalozi mdogo wa Marekani katika mji wa kusini mgharibi mwa nchi hiyo wa Chengdu jana Ijumaa, ikiwa ni ulipizaji kisasi wa haraka kutokana na kufungwa kwa ubalozi wake mdogo mjini Houston.
Wiki mbili zilizopita, waziri wa mambo ya kigeni wa China Wang Yi alikuwa kijiuliza iwapo mahusiano hayo yanaweza kubakia kuwa katika njia ya kawaida. Siku ya Alhamis, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alitoa jibu. Alisema muda umewadia kubadilisha mwelekeo.
"Dhana ya kale ya mahusiano ya kuifumbia macho China haitawezekana," alisema katika hotuba katika maktaba ya rais Richard Nixon huko katika eneo la kusini mwa Califonia. "Hatupaswi kuendelea nayo. Hatulazimiki kuirejea."
Amri ya kuufunga ubalozi mdogo mjini Chengdu, katika jimbo la kusini magharibi mwa China , kunaonekana kama jibu kwa mujibu wa athari na kiwango, ikiendeleza utaratibu wa China wa jibu la jino kwa jino kwa hatua za Marekani.
Athari ya hatua za Marekani kwa China
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Wang Wenbin alisema.
"Julai 21 Marekani ilifanya uchokozi kwa kudai ghafla kuwa China ifunge ubalozi wake mdogo mjini Houston. hatua hiyo ya Marekani inakiuka sheria za kimataifa, misingi ya utaratibu wa mahusiano ya kimataifa, na masharti ya makubaliano ya kibalozi kati ya China na Marekani. Hatua hiyo imeathiri kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya China na Marekani."
Ilikuwa ziara ya Nixon nchini China mwaka 1972, ikiwa ni ziara ya kwanza kufanywa na rais wa Marekani tangu wakomunisti waingie madarakani mwaka 1949, iliweka kando kiasi utaratibu wa vita baridi na kusafisha njia kwa ajili ya kurejesha mahusiano mwaka 1979.
Marekani imekuwa mshirika wa karibu wa kiongozi wa wakati huo Chiang Kai-shek katika vita vikuu vya pili vya dunia na kwa muda wa miongo mitatu iliitambua Taiwan kama serikali ya China baada ya Chiang kukimbilia huko wakati alipopoteza mpambano wa udhibiti wa China bara dhidi ya Wakomunist mwaka 1949.
Mahusiano baina ya Marekani na serikali ya kikomunist mjini Beijing yalianza kudhoofika katika miaka ya 1970, wakati mahusiano ya China na Urusi ya Umoja wa Kisovieti yalipoporomoka na kiongozi mkuu Mao Zedong alipohitaji nguvu mbadala kwa jirani yake huyo ambaye ni mwenye nguvu.
Kiongozi mpya , Deng Xiaoping, alifanya ziara nchini Marekani mwaka 1979 baada ya kuanzishwa mahusiano ya kidiplomasia, akipiga picha na kutabasamu huku akivalia kofia maarufu inayovaliwa na wachunga ng'ombe mjini Houston. Ubalozi ambao unafungwa mjini humo ulifunguliwa baadaye mwaka huo huo. Ulikuwa ubalozi wa kwanza wa China nchini Marekani.
Wizara ya mambo ya kigeni ya China ilisema jana kuwa hotuba aliyotoa waziri wa mambo ya kigeni Mike Pompeo kuhusu China haikutilia maanani uhalisia na ilijaa tu chuki za kinadharia.
Wang Wenbin , msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni aliwaambia waandishi habari mjini Beijing kuwa China inaitaka Marekani kutupilia mbali , "fikira za vita baridi.