JamiiChina
China yaanza kulegeza masharti ya kukabiliana na UVIKO-19
13 Desemba 2022Matangazo
Hatua hiyo inatazamiwa kupunguza uwezekano wa watu kulazimishwa kukaa karantini baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika kwa maambukizo.
Uamuzi huo ni sehemu ya mkakati wa Beijing kuondokana na sera yake ya kuzuia kabisa maambukizo ya virusi vya Korona, ambayo imekumbana na upinzani na maandamano makubwa ya umma.
Kwa mara ya kwanza, maandamano yalishuhudiwa kwenye miji kadhaa ya China, ambapo waandamanaji walimtaka Rais Xi Jinping ajiuzulu.
Wiki iliyopita, mamlaka nchini humo zilitangaza kufutwa kwa amri ya kujifungia ndani na kulegeza masharti makali ya kufanya vipimo.
Pia ziliwaruhusu wale wenye dalili za kawaida za maambukizo kusalia nyumbani, badala ya kuwekwa kwenye vituo maalum vya karantini.