China yaapa kulinda maslahi yake baada ya kitisho cha Trump
22 Januari 2025China imetangaza Jumatano kuwa italinda maslahi yake ya kitaifa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza kwamba ushuru wa forodha wa asilimia 10 kwa bidhaa za China ungetekelezwa kuanzia Februari mosi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, alifafanua msimamo huo akisema kwamba taifa hilo linaamini hakuna mshindi katika vita vya kibiashara au ushuru, hivyo litaendelea kulinda maslahi yake.
Soma pia: China yaonya vita vya biashara na Umoja wa Ulaya
Aidha, Trump alieleza kuwa kuna haja ya kurekebisha uwiano wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, akidai umoja huo haununui bidhaa za kutosha za Marekani, na hivyo angetafuta suluhisho kwa kuongeza ushuru au kuishawishi Ulaya kununua zaidi mafuta na gesi kutoka Marekani.