1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaapa kulinda ulinzi wa pamoja wa kiusalama na Urusi

3 Novemba 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema nchi yake inataka kuimarisha mahusiano yake na Urusi na kutetea masilahi yao ya pamoja ya kiusalama.

China Hangzhou 2025 | Li Qiang na Mikhail Mishustin.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwa na mwenzake wa Urusi Mikhail Mishustin. Picha: Dmitry Astakhov/AP Photo/picture alliance

Aliyasema hayo wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Urusi nchini humo Mikhail Mishustin. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika mjini Hangzhou, Li amesema Urusi na China ni marafiki na washirika wazuri wanaoaminiana.

Mishustin yupo katika ziara ya siku mbili China ambako shirika la habari la taifa TASS limesema hapo kesho waziri mkuu huyo atakuwa na mazungumzo na rais  Xi Jinping.

Mazungumzo yao yanatarajiwa kutuwama katika masuala ya Uchumi na ushirikiano wa teknolojia, wakati Urusi ikijaribu kukabiliana na vikwazo vya Magharibi kufuatia vita vyake Ukraine na China nayo ikivutana na Marekani kuhusu masuala ya kibiashara na kiteknolojia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW