China inavutana na Marekani
18 Septemba 2018Kiwango hicho cha ushuru kilichotangazwa na Rais Trump kinatarajiwa kuanza kutekeleza wiki ijayo. Pamoja na hatua hiyo ametangaza pia kuzifanyia ukaguzi bidhaa zote za China, zinazoingizwa nchini Marekani. Katika taarifa yake ya jana Jumatatu Trump amenukuliwa akisema "Kwa miezi kadhaa, tumeitaka China kuifanyika marekebisho hii hali ya kibiashara isiyo ya haki na kuyatendea haki makampuni ya Kimarekani."
Trump aendelea kuitisha China
Katika taarifa hiyo, Trump aliendeleo kuisema kuwa China haioneshi nia ya kutaka kubadili mwenendo wake, ukiwemo wa wizi na kuhamisha teknolojia. Utozaji ushuru wa sasa wa asilimia 10 la Marekani kwa bidhaa za China ambalo linadumu hadi mwishoni mwa mwaka huu, viwango vyake vinatarajiwa kuongezeka hadi kufikia asilimaia 25. lakini Chen Fayi, mwanajeshi mstaafu nchini China anasema "Nadhani Trump atabadilika, Hana muda mrefu wa kuendelea. Sasa amefikia mwisho wake"
Katika taarifa ya hivi punde ya waziri wa biashara wa China, inasema "ili kulinda haki na maslahi na utaratibu wa haki wa kibiashara wa kimataifa, China haina la kukwepa isipokuwa kupima hatua za kuchukua kwa lengo la kuendana na hali ya sasa kibiashara."Taarifa hiyo haijataja kitisho cha awali cha serikali ya China cha kutangaza kodi kwenye kadhaa za Marekani za thamani ya karibu dola bilioni 60, endapo Marekani itaendelea na kuendeleza na wimbi lake la nyongeza za kodi.
Katika utaratibu wake wa kawaida wa taarifa kwa umma msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Geng Shuang amesema china itatangaza hatua madhubuti itakayozichukua kwa wakati muafaka, kwa kuongeza kusema hatua za upande mmoja zinazochukiwa na Marekani kwa lengo la kujikinga kibiashara hazikubaliki kwa upande wa China. Hata hivyo tayari Trump alikwishasema ikiwa China itachukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya wakulima wao au hata viwanda vingine vyovyote, kwa haraka sana watakeleza awamu nyingine ya watu, ambayo viwango vyake vya ushuru vinakadiria kufikia dola bilioni 267 kwa bidhaa wanazozipokea kutoka China.
Lakini utozaji mpya wa ushuru wa Marekani kwa kiasi kikubwa lutavikumba vifaa vya kieletroniki zikiwemo nyenzo za data za sauti, vifaa vya kuhifadhi kumbukumbu vya kompyuta, pamoja na vifaa vya maofisini kama vya kunakili kumbukumbu na vinginevyo vinavyofanana na hivyo.
Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman