1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaapa kuangamiza majaribio ya uhuru wa Taiwan

28 Novemba 2024

China imeapa kuyaangamiza kabisa majiribio yoyote ya uhuru wa Taiwan. Hii ni wakati Rais wa kisiwa hicho kinachojitawala Lai Ching-te akijiandaa kuanza ziara ya kigeni.

China | Wu Qian
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Wu Qian Picha: Chen Boyuan/HPIC/dpa/picture alliance

Akijibu swali kuhusu iwapo jeshi la China litachukua hatua za kukabiliana na ziara ya Lai ya eneo la Pasifiki, msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Wu Qian alisema wanapinga vikali uhusiano rasmi na eneo la Taiwan la China kwa namna yoyote ile.

Beijing inadai kisiwa cha Taiwan kuwa sehemu ya himaya yake na inapinga uhusiano wowote ambao Taipei inaanzisha na nchi nyingine.

Rais wa Taiwan Lai kuanzia Jumamosi atazuru Hawaii na mkoa wa Guam unaomilikiwa na Marekani wakati wa ziara yake ya mataifa matatu ya eneo la Pasifiki. Ni ziara yake ya kwanza ya kigeni tangu alipochukua uongozi mwezi Mei. 

China: Tuko tayari kusambaratisha hatua zozote za kuipatia Taiwan uhuru

Wakati huo huo, jeshi la Taiwan mapema limefanya mazoezi likitumia ndege, manowari na mifumo ya ulinzi wa makombora. Hayo ni wakati wizara yake ya ulinzi ikiripoti kugunduliwa kwa maputo mawili ya China karibu na kisiwa hicho.

Beijing aghalabu hurusha ndege za kijeshi, droni na manowari za kivita, na mara kwa mara maputo, karibu na Taiwan wakati ikiongeza mbinyo wa kijeshi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW