1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yafanya luteka ya ´onyo´ kuzunguka Taiwan

19 Agosti 2023

China, leo imezindua luteka ya kijeshi karibu na Taiwan kama ishara ya onyo kali baada ya kuelezea kukasirishwa na ziara ya muda mfupi iliyofanywa na makamu wa rais wa kisiwa hicho William Lai nchini Marekani.

China hält Militärübung nahe Taiwan ab
Meli na ndege za kivita za China zimeonekana kwenye ujia wa maji wa Taiwan Picha: CCTV/AP/dpa/picture alliance

Lai, mgombea anayeoongoza kuelekea uchaguzi wa rais wa Taiwan utakaofanyika mwakani na mkosoaji mkubwa wa China, alirejea jana kutoka ziara yake nchini Paraguay ambayo alipokuwa njiani alisimama kwa muda mjini New York na San Francisco.

China iligadhabishwa na hatua hiyo ya Lai na kuelezea kwa mara nyingine kwamba mwanasiasa huyo ni msumbufu na kuapa kuchukua hatua thabiti.

Taiwan kwa upande wake pia imethibitisha taarifa za China kufanya mazoezi ya kijeshi ikisema ndege za kivita zipatazo 42 zimeshuhudiwa katika anga lake.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imelaani mazoezi ya kijeshi ya China na kuyataja kuwa ni tabia ya kichokozi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW