1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yafanya "mashambulizi ya kutishia" dhidi ya Taiwan

24 Mei 2024

China imefanya mifano ya mashambulizi ya makombora mapema leo wakati wa luteka zake za siku mbili dhidi ya Taiwan.

Taiwan | China
Meli za kivita za jeshi la majini la China kwenye luteka ya kijeshi dhidi ya Taiwan.Picha: Taiwan Defence Ministry/Handout/REUTERS

Kulingana na kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali ya China, CCTV, kwenye luteka hizo China iliwapeleka pia washambuliaji waliokuwa wamebeba makombora na kufanya kile kilichoitwa "mashambulizi ya kutishia" katika pwani ya Taiwan kwa ushirikiano na wanajeshi wa majini.

China imesema imeanzisha luteka hizo kumuadhibu rais mpya wa Taiwan, Lai Ching-te, na inajaribu uwezo wake wa "kunyakua madaraka" na kudhibiti maeneo muhimu ya Taiwan.

Soma zaidi: Taiwan 'itatetea maadili ya uhuru na demokrasia"
 
Luteka hizo zilianza siku tatu tu baada ya Rais Lai wa Taiwan kuapishwa.

China inachukulia Taiwan iliyo na mamlaka yake ya ndani kama himaya yake na inampinga Lai kama anayechochea utengano.

Taiwan imelaani vikali luteka hizo na kuitaka China kuacha uchokozi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW