1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asia

China yaionya Marekani dhidi ya kuiunga mkono Ufilipino

Sylvia Mwehozi
28 Agosti 2024

Mwanadiplomasia wa juu wa China Wang Yi amemuonya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan aliye ziarani nchini humo, juu ya kuiunga mkono Ufilipino Bahari inayozozaniwa ya Kusini mwa China.

China Peking | Jake Sullivan na Wang Yi
Mwanadiplomasia wa juu wa China Wang Yi na Mshauri wa usalama wa Marekani Jake SullivanPicha: Ng Han Guan/AP Photo/picture alliance

Mwanadiplomasia wa juu wa China Wang Yi amemuonya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani Jake Sullivan aliye ziarani nchini humo, juu ya kuiunga mkono Ufilipino Bahari inayozozaniwa ya Kusini mwa China.

"Marekani haipaswi kutumia mikataba ya nchi mbili kama kisingizio cha kudhoofisha mamlaka na uadilifu wa ardhi ya China, wala haipaswi kuunga mkono vitendo vya ukiukaji vya Ufilipino," alisema Wang wakati alipokutana na Sullivan kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali CCTV.

Sullivan alitua katika mji mkuu wa China siku ya Jumanne kwa ziara ya siku tatu, akisema anatazamia "mazungumzo yenye tija" na waziri wa mambo ya nje Wang.

Washirika wa Washington Japan na Ufilipino wameilaumu China wiki iliyopita kwa kuibua mvutano wa kikanda, huku Tokyo ikiishutumu Beijing kwa kukiuka anga yake na Manila ikisema ni "mvurugaji mkubwa zaidi" wa amani Kusini-mashariki mwa Asia.

Kwa mujibu wa CCTV, Wang amemsisitizia Sullivan kwamba "China ina nia thabiti ya kulinda mamlaka yake ya eneo na haki za bahari juu ya visiwa vya Bahari ya Kusini ya China".Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani Jake Sullivan anaitembelea China

Mvutano kati ya Manila na Beijing kuhusu miamba na eneo linalozozaniwa katika Bahari ya China Kusini umeongezeka katika siku za hivi karibuni.

Beijing ilisema Jumatatu ilikuwa imechukua "hatua za udhibiti" dhidi ya meli mbili za walinzi wa pwani ya Ufilipino ambazo ziliingia ndani ya maji "kinyume cha sheria".

Manila ilisema meli za China zimezuia meli za Ufilipino kusambaza tena meli zao za walinzi wa pwani katika eneo hilo, na kusema kuwa hatua hiyo ni "uchokozi" na kuiita Beijing "mvurugaji mkubwa" wa amani Kusini-mashariki mwa Asia.Ufilipino na China zafikia makubaliano kuzima mgogoro

Sullivan na Wang wamekutana mara tano katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita huko Washington, Vienna, Malta na Bangkok, pamoja na Rais wa Marekani Joe Biden na kiongozi wa China Xi Jinping katika mkutano wa kilele wa Novemba 2023 huko California.

 

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW