1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

China yaionya Marekani, Korea Kusini kuhusu nyuklia

27 Aprili 2023

China imeionya Marekani, Korea Kusini dhidi ya kuchochea makabiliano na Korea Kaskazini, baada ya Joe Biden na Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini kusema utawala wa Pyongyang utafikia mwisho iwapo utatumia silaha za nyuklia

 USA Südkorea | Joe Biden und Yoon Suk Yeol
Picha: Yonhap/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning amesema pande zote zinatakiwa kukabiliana na kiini cha mvutano katika rasi ya Korea na kuchukua jukumu la kuhamasisha makubaliano kwa njia ya amani, huku akionya dhidi ya hatua za makusudi zinazochochea wasiwasi.

Kwenye mkutano wa kilele mjini Washington, Biden na Yoon Suk Yeol waliweka wazi kwamba ikiwa utawala wa Korea Kaskazini utaishambulia Korea Kusini na Marekani unaweza kukabiliwa na majibu makali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW