China yaionya Marekani kuhusu kupeleka meli ya kivita
24 Machi 2023China imedai hatua hiyo ya Marekani inakiuka uhuru wa mamlaka yake na usalama. Onyo la China limekuja wakati ambapo mivutano inaongezeka kati ya nchi hiyo na Marekani katika eneo hilo.
Marekani inazidi kuchukuwa hatua ya kudhibiti kujitanua kwa China katika eneo la bahari ya Kusini mwa China, eneo la kimkakati ambalo China inadai ni himaya yake. Jana, baada ya Marekani kupeleka meli ya kivita ya USS Milius yenye uwezo wa kuharibu makombora karibu na visiwa vya Paracel, China ilisema jeshi lake la wanamaji na la anga liliitimua meli hiyo, madai ambayo yamekanushwa na jeshi la Marekani.
Soma pia: China: Meli ya kivita ya Marekani imevuka mipaka yake
Leo Ijumaa, Marekani imepeleka tena meli hiyo kwenye eneo hilohilo ambalo pia Vietnam na Taiwan zinadai zina umiliki.