1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaishtumu Marekani kwa shambulizi la mtandaoni

19 Oktoba 2025

China imeishtumu idara ya Usalama wa Kitaifa ya Marekani kwa kutekeleza shambulizi la mtandao kwenye kituo chake cha kitaifa cha Kusimamia usahihi wa saa kwa sekta kama vile za mawasiliano.

China Peking | Rais wa China
Rais wa China Xi JinpingPicha: Maxim Shemetov/REUTERS

China imesema uharibifu wowote unaohusiana na taasisi kama, fedha, nishati, usafiri na ulinzi kufuatia utafiti uliofanywa, ungeweza kuvuruga mawasiliano ya mtandao, mifumo ya fedha nausambazaji wa nishati.

Katika chapisho kwenye mtandao wa WeChat, wizara ya usalama wa nchi, imedai kwamba idara hiyo ya Marekani ilitumia udhaifu katika huduma za kutuma ujumbe kupitia kampuni moja ya mawasiliano ya simu kuiba taarifa nyeti kutoka vifaa vya wafanyikazi wa kituo hicho cha China mnamo 2022.

Hata hivyo haikufafanua ni kampuni gani.

Wizara hiyo pia imesema idara hiyo ya Marekani, ilitumia aina 42 za vifaa maalumu vya mashambulizi ya mtandao kulenga mifumo mbali mbali ya taasisi hiyo ya China kupenyeza mfumo muhimu wa kudhibiti nyakati rasmi kati ya 2023 na 2024.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW