SiasaCuba
China yaitaka Marekani kuacha kuiandama Cuba
21 Mei 2026
Matangazo
Akizungumza leo Alhamisi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Guo Jiakun, amesema Washington inapaswa kuacha kutumia vikwazo na mfumo wa sheria kama nyenzo za kuishinikiza Cuba na kuacha vitisho vya matumizi ya nguvu.
Serikali ya Rais Donald Trump jana Jumatano ilitangaza shutuma hizo dhidi ya Castro kwamba alihusika na tukio la mwaka 1996 ambapo ndege mbili za kiraia za kundi la wakimbizi wa Cuba lenye makao yake Miami zilidunguliwa na jeshi la Cuba, na kusababisha vifo vya watu wanne.
Hatua hiyo imezidisha mzozo kati ya Washington na Havana, wakati utawala wa Trump ukiendelea kuongeza shinikizo la kiuchumi na kisiasa dhidi ya serikali ya kikomunisti ya Cuba.