1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yaituhumu Marekani kuigeuza Taiwan kuwa eneo hatari

5 Julai 2023

Wizara ya Ulinzi ya China imesema Marekani inaifanya Taiwan kuwa eneo hatari kwa hatua yake ya hivi karibuni ya kuidhinisha mauzo ya silaha na zana za kijeshi.

Tan Kefei I China
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Tan Kefei Picha: Heng Sinith/AP Photo/picture alliance

Wizara ya Ulinzi ya China imesema Marekani inaifanya Taiwan kuwa eneo hatari kwa hatua yake ya hivi karibuni ya kuidhinisha mauzo ya silaha na zana za kijeshi kwa kisiwa hicho kinachojitawala ambacho Beijing inadai kuwa sehemu ya himaya yake.

Matamshi hayo ya China yanafuatia mauzo ya silaha zenye thamani ya dola milioni 440.2 yaliyofanywa na Washington kwa Taiwan ikijumuisha makombora na vipuri kwa ajili ya magari ya kijeshi ,mifumo ya ulinzi, vifaa vingine vya usalama.

Soma zaidi:Manowari za China zakatiza ujia wa Bahari wa Taiwan

Msemaji wa wizara hiyo Kanali Tan Kefei ameituhumu Washington kuwa inapuuza wasiwasi wa China kuhusu Taiwan na inakiweka kisiwa hicho katika hali ya hatari inayoweza kugeuka kuwa janga.

Suala la hadhi ya Taiwan limekuwa moja ya sababu za mivutano kati ya Washington na Beijing, na China imepinga mara zote mauzo ya silaha yanayofanywa na Marekani kwa kisiwa hicho.