1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaAsia

China yakabiliwa na ongezeko la magonjwa ya mfumo wa kupumua

24 Novemba 2023

China imesema hakuna vimelea vipya vya maradhi vilivyogunduliwa lakini imewataka raia wake kuwa waangalifu kutokana na ongezeko la visa vya magonjwa ya mfumo wa kupumua vinavyoripotiwa sehemu mbalimbali nchini humo.

Watu wakisubiri kumuona daktari katika moja ya hospitali China
Watu wakisubiri kumuona daktari katika moja ya hospitali ChinaPicha: CFOTO/picture alliance

Shirika la Afya Ulimwenguni limezitaka mamlaka za Beijing kutoa takwimu kuhusu magonjwa hayo.

Visa vya magonjwa ya kupumuavimeripotiwa kuongezeka China hasa katika maeneo ya kaskazini kama mji mkuu Beijing na mkoa wa Liaoning wakati huu msimu wa baridi ukianza.

Soma pia:WHO yatala data za ugonjwa hatari wa kupumua

Mamlaka za China zimeonya kuhusu kuongezeka kwa mafua, homa ya mapafu na maambukizi ya UVIKO-19.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW