China yamuwekea vikwazo Balozi wa Taiwan nchini Marekani
7 Aprili 2023Beijing imepiga pia marufuku wawekezaji na makampuni ya Balozi huyo kushirikiana na mashirika ya China na hata watu binafsi.
Hayo yanajiri baada ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen kuikasirisha Beijing kwa kukutana wiki hii mjini Los Angeles na Spika wa Bunge la Marekani Kevin McCarthy.
Soma pia: Rais wa Taiwan akutana na spika wa bunge la Marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza pia hatua dhidi ya Taasisi ya Hudson ya Marekani na Maktaba ya Reagan pamoja na viongozi wake wakuu, wakisema taasisi zote mbili zilitoa jukwaa na vifaa kwa kile walichokiita shughuli za kujitenga za Rais Tsai.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Taiwan imejibu kwa ghadhabu hatua hiyo ikisema China haina haki ya kuingilia safari za rais Tsai na kwamba Beijing inajidanganya ikiwa inafikiri kuwa vikwazo hivyo vingekua na athari yoyote.