Migogoro
China yaonya juu ya vita Taiwan baada ya luteka za kijeshi
25 Mei 2024Matangazo
China imeonya kuhusu vita juu ya Taiwan na kusema itaongeza hatua za makabiliano hadi muungano kamili upatikane, baada ya vikosi vya jeshi la China kukamilisha luteka karibu na kisiwa hicho kinachojitawala.
Meli na ndege za kivita ziliizingira Taiwan kwa siku ya pili ya luteka ambazo Beijing ilisema zilikuwa majaribio ya uwezo wake wa kukamata kisiwa hicho, siku chache baada ya rais mpya kuapishwa.
Soma pia: Taiwan 'itatetea maadili ya uhuru na demokrasia"
Msemaji wa wizara ya Ulinzi ya China Wu Qian, alisema jana kuwa Rais mpya waTaiwan, Lai Ching-te amepinga kanuni ya China moja na kuwaweka wakaazi wa Taiwan katika hali ya vita na hatari.
Wakati wa kuapishwa kwake, Lai alitoa hotuba ambayo China iliilaani na kuifafanisha na kutangaza uhuru.