1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yaonya vita vya biashara na Umoja wa Ulaya

21 Juni 2024

China imeonya hivi leo kwamba hatua za Umoja wa Ulaya kuzidisha msuguano wa kibiashara zinaweza kuzusha vita vya kiuchumi kati ya Beijing na Umoja huo.

Rais wa Xi Jinping wa China na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.
Rais wa Xi Jinping wa China na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa.Picha: Kiran Ridley/Getty Images

Wizara ya biashara ya China imesema Umoja wa Ulaya ndio utawajibishwa ikiwa hilo litatokea, lakini ikasisitiza kuwa na matumaini ya kusuluhisha tofauti zao kwa njia ya mazungumzo na kuepusha tatizo hilo kutanuka zaidi.

Soma zaidi: Je, EU inaanzisha vita vya biashara na China

Wiki iliyopita, Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya ilipendekeza ushuru wa hadi asilimia 38.1 kwa magari ya umeme yanayoagizwa kutoka China.

Beijing ilipinga vikali hatua hiyo ambayo ilisababisha mkwaruzano wa mahusiano ya kibiashara na kuhatarisha hatua za kulipiza kisasi kutoka China, taifa la pili kwa uchumi mkubwa duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW