1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

China yapinga vikwazo vya Marekani dhidi ya mafuta ya Iran

Saleh Mwanamilongo
2 Mei 2026

Wizara ya Biashara ya China imesema hatua hizo za Marekani hazitambuliki wala kutekelezwa, ikidai zinakiuka sheria za kimataifa na kanuni za uhusiano wa kimataifa.

Indien | Mumbai 2026 – LPG‑Tanker „Jag Vasant“ im Hafen von Mumbai
China yapinga vikwazo vya Marekani dhidi ya viwanda vya mafuta vinavyohusiana na IranPicha: Punit Paranjpe/AFP

China imesema haitazingatia vikwazo vya Marekani dhidi ya kampuni tano za Kichina zinazotuhumiwa kununua mafuta kutoka Iran. Wizara ya Biashara ya China imesema hatua hizo za Marekani hazitambuliki wala kutekelezwa, ikidai zinakiuka sheria za kimataifa na kanuni za uhusiano wa kimataifa.

Marekani imekuwa ikiimarisha vikwazo dhidi ya Iran kwa lengo la kupunguza mapato yake ya mafuta, huku China ikiwa mmoja wa wanunuzi wakuu wa mafuta hayo kupitia viwanda vidogo vya kusafisha mafuta.

Hata hivyo, Beijing imesisitiza kupinga vikwazo vya upande mmoja visivyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa. Wakati huo huo, mvutano kati ya Washington na Tehran unaendelea bila suluhu ya kudumu, huku Rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping baadaye mwezi huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW