1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yaruhusu wanandoa kupata watoto watatu

31 Mei 2021

Shirika la habari la China linaripoti kuwa chama cha Kikomyunisti cha China kitalegeza msimamo na kuwakubalia wanandoa kupata watoto watatu badala ya wawili kutokana na idadi ya wazee inayoongezeka nchini humo.

China Familie mit Baby in Nanjing
Picha: picture-alliance/dpa/Yu Ping

Shirika la habari la China linaripoti kuwa chama cha Kikomyunisti cha China kitalegeza msimamo na kuwakubalia wapenzi kuzaa watoto watatu badala ya wawili kutokana na idadi ya wazee inayoongezeka nchini humo.

Tangazo hilo linafuatia takwimu za sensa zilizoonyesha kuwa idadi ya Wachina walio katika umri wa kufanya kazi imepungua katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita huku idadi ya watu walio na zaidi ya umri wa miaka 65 ikiwa imeongezeka. Jambo hili limewekea shinikizo dhidi ya uchumi na jamii.

Chama hicho tawala cha China kiliweka vikwazo vya idadi ya watoto kwa wazazi tangu 1980 ili kudhibiti idadi ya watu nchini humo. Mwaka 2015 vikwazo vya wazazi kuwa na mtoto mmoja viliondolewa na idadi hiyo ikaongezwa na wazazi wakakubaliwa kuwa na watoto wawili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW