1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

China yapinga Taiwan kukutana na viongozi wa Marekani

29 Machi 2023

China imesema leo Jumatano kwamba itachukua hatua iwapo Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen atakutana na spika wa Bunge la Marekani wakati wa safari yake katika nchi za Amerika ya kati kupitia nchini Marekani.

Taiwan Taoyuan | Präsidentin Tsai Ing-wen vor der Abreise in die USA
Picha: Ann Wang/REUTERS

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen amesema shinikizo kutoka mataifa ya nje halitatishia azimio la nchi yake la kuendelea kuwasiliana na ulimwengu. Rais huyo wa Taiwan Tsai Ing-wen ameondoka Jumatano kuelekea Amerika ya Kati kupitia Marekani anakwenda Guatemala na Belize nchi iliyo kwenye pwani ya kaskazini-mashariki ya Amerika ya Kati.

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wenPicha: Sam Yeh/AFP/Getty Images

Lengo la ziara ya kiongozi huyo wa Taiwan ni kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi hizo washirika. Rais Tsai akiwa njiani kurudi Taiwan atasimama mjini California, ambapo anatarajiwa kukutana na Spika wa Bunge la Marekani Kevin McCarthy.

China kwa upande wake imetoa angalizo kwamba hairidhishwi na mpango huo wa Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen kukutana na spika wa Bunge la Marekani wakati wa safari yake hiyo. China inakichukulia kisiwa hicho kinachojitawala kama ni kisiwa kilichoasi na kwamba kisiwa chaTaiwan kinastahili kuwemo kwenye eneo la China na mara kwa mara kwa mara imeionya Marekani juu kukutana na kiongozi wa Taiwan jambo ambalo China inasema itaonekana kana kwamba Taiwan ni nchi tofauti.

Soma:Rais wa zamani wa Taiwan aitembelea China

Wiki iliyopita nchi hiyo iliwasilisha pinganizi lake kwa Marekani kuhusu kusimama kwenye baadhi ya miji ya Marekani kiongozi huyo wa Taiwan ambapo Marekani ilijibu tu kwamba ziara hiyo ilishapangwa tangu awali. Safari za rais wa Taiwan za kimataifa kupitia Marekani zimekuwa za kawaida kwa miaka mingi, wamesema maafisa wakuu wa Marekani.

Kushoto: Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen. Kulia: Rais wa China Xi Jinping.Picha: TAIWAN PRESIDENTIAL OFFICE/REUTERS | THOMAS PETER/REUTERS

Safari ya Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen inafanyika wakati ambapo uhusiano wa Marekani na China uko katika kile kiwango kibaya zaidi tangu Washington iliporekebisha uhusiano wake na Beijing mnamo mwaka 1979 na kubadili msimamo wake wa kuitambua Taipei kidiplomasia.

Hata hivyo Marekani inasalia kuwa mshirika muhimu zaidi wa kimataifa wa Taiwan na msambazaji wake mkubwa wa silaha Kisiwa chaTaiwan ni suala nyeti zaidi la eneo la China na ndio chanzo cha mzozo mkubwa kati ya nchi hiyo na Marekani. Nchi nyingi zinadumisha uhusiano usio rasmi na Taiwan.

Vyanzo: AFP/RTRE/AP