SiasaAsia
China kutuma mjumbe maalum Ukraine na nchi za Ulaya
12 Mei 2023Matangazo
Hatua hiyo itakuwa ni ya kwanza ya nchi hiyo kupeleka mwanadiplomasia wake wa ngazi ya juu katika nchi hiyo ya Ukraine inayokabiliwa na vita tangu Urusi ilipofanya uvamizi wake mwaka jana. Beijing imesema kwamba aliyekuwa balozi wake nchini Urusi kuanzia mwaka 2009 mpaka 2019 Li Hui ataongoza ujumbe wa kuelekea Ukraine.
Soma zaidi:Simu ya Rais Xi wa China kwa Zelensky ina tija gani?
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang Wenbin ameuambia mkutano wa waandishi wa habari leo Ijumaa kwamba lengo la ziara ya Li ambaye ni mjumbe maalum wa China kuhusu masuala ya Ulaya na Asia, nchini Ukraine, Poland, Ufaransa, Ujerumani na Urusi ni kuzungumza na pande zote kuhusu suala la kuumaliza mgogoro wa Ukraine kwa njia za kisiasa.