1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China yatahadharisha kuhusu mivutano kati yake na Marekani

8 Machi 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ametahadharisha kuhusu hatari ya China kutokuelewana na Marekani akisema hilo litapelekea migogoro na makabiliano ambayo yanaweza kuitumbukiza dunia nzima katika janga.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang YiPicha: Mandel Ngan/AP/picture alliance

Wang Yi ameitoa kauli hiyo Jumapili kabla ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuwa anatarajia mwishoni mwa mwezi huu kuitembelea China. Trump na rais wa China Xi Jinping walikutana mara ya mwisho Korea Kusini mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, kabla ya mkutano wa kilele wa jukwaa la Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki (APEC), ambapo walikubaliana miongoni mwa mambo mengine, kusitisha kwa muda mzozo wao unaoendelea wa kibiashara.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa huenda Beijing ikaahirisha ziara hiyo kutokana na shambulio la Marekani dhidi ya Iran, ambayo ni moja ya washirika wakuu wa kiuchumi wa China.  Wang Yi amelaani mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran  akisisitiza kuwa dunia haipaswi kuongozwa na "sheria ya mwenye nguvu" na kwamba hakukuwa na uungwaji mkono wa umma ili kubadili utawala nchini Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW