China yataka usalama wa Bongo uhakikishwe
30 Agosti 2023China leo imetoa wito kwa pande zote nchini Gabon kuhakikisha usalama wa Rais Ali Bongo baada ya kundi la majeshi kutangaza kwamba wanaufikisha mwisho muhula wake. Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Wenbin amesema China inafuatilia kwa karibu hali ilivyo nchini Gabon.
Wakati huo huo Ufaransa kupitia Waziri Mkuu Elisabeth Borne inasema Ufaransa inafuatilia hali inavyoendelea nchini humo. Tamko hili la Borne ndilo la kwanza kutoka Ufaransa ambayo ni mkoloni wa zamani wa Gabon.
Hayo yanafanyika wakati ambapo mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya wamesema watajadiliana kuhusiana na hali nchini Gabon. kulingana na mkuu wa sera za kigeni wa umoja huo Josep Borrell, iwapo mapinduzi yatathibitishwa, basi hali ya usalama itazidi kuyumba katika eneo hilo.