1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yatangaza mpango wa kupunguza uzalishaji gesi chafu

25 Septemba 2025

China imetangaza kwa mara ya kwanza malengo ya kupunguza gesi zinazochochea ongezeko la joto duniani, ikiwa ni hatua muhimu kutoka taifa linaloongoza kwa uchafuzi wa mazingira duniani.

Uchafuzi wa hewa nchini China
Gesi taka kutoka kwenye bomba la moshi katika mji wa Changchun, kaskazini mashariki mwa China mkoani Jilin.Picha: picture-alliance/AP/Imaginechina

China imetangaza kwa mara ya kwanza malengo ya kupunguza gesi zinazochochea ongezeko la joto duniani, ikiwa ni hatua muhimu kutoka taifa linaloongoza kwa uchafuzi wa mazingiraduniani.

Tangazo hilo lilitolewa kwa njia ya video na Rais wa China Xi Jinping katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ambapo takriban mataifa 120 yanawasilisha mipango ya kupunguza ongezeko la joto duniani, ambalo linasababisha majanga kama mafuriko na moto mkubwa wa nyika.

Kwa mujibu wa mpango mpya, China itapunguza uzalishaji wa gesi chafu kwa asilimia 7 hadi 10 ifikapo mwaka 2035. Wachambuzi wamesema ingawa kiwango hicho kinaweza kuonekana kuwa kidogo, China ina historia ya kuweka malengo ya chini lakini kuyatimiza kwa kiwango kikubwa, hasa kutokana na maendeleo makubwa katika teknolojia rafiki kwa mazingira.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW