China yatangaza 'ushirikiano wa kimkakati' na Syria
22 Septemba 2023Matangazo
Xi amesema hayo wakati wa mazungumzo na rais wa Syria Bashar al-Assad anayetafuta msaada wa kifedha kusaidia kuijenga upya nchi yake iliyoharibiwa na machafuko.
Kulingana na taarifa iliyosomwa na shirika la habari linalomilikiwa na China CCTV, Xi alisema ushirikiano huo utakuwa hatua muhimu katika historia ya uhusiano wa nchi hizo mbili, lakini bila ya kutoa maelezo zaidi.
Viongozi hao wamekutana katika mkesha wa sherehe za ufunguzi wa michezo ya bara la Asia, ambayo Assad atahudhuria kama sehemu ya ziara yake ya kwanza nchini China tangu mwaka 2004.