1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yatishia kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa Taiwan

12 Oktoba 2024

China imetishia kuichukulia hatua Taiwan kwa kuiwekea vikwazo vya kibiashara ikiwa ni siku mbili tu baada ya Beijing kuikosoa hotuba ya rais wa Taiwan, Lai Ching -Te.

Taiwan Feierlichkeiten zum Nationalfeiertag | Präsident Lai Ching-te
Rais wa Taiwan, Li ching-TePicha: Ann Wang/REUTERS

China imetishia kuichukulia hatua Taiwan kuiwekea vikwazo vya kibiashara ikiwa ni siku mbili tu baada ya Beijing kuikosoa hotuba ya rais wa Taiwan, Lai Ching -Te.

Mapema leo Jumamosi wizara ya biashara ya China imesema kuwa inaweza kuongeza ushuru na kukiwekea vikwazo vya kiuchumi kisiwa hicho katika siku zijazo.

Soma zaidi. China, Japan zadhamiria kuimarisha uhusiano

Alhamisi wiki hii katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya kitaifa, Rais wa Taiwan alisema Jamhuri ya Watu wa China haina haki ya kuiwakilisha Taiwan lakini kisiwa hicho kiko tayari kufanya kazi na Beijing kupambana na changamoto kama vile mabadiliko ya tabia nchi.

Kauli hiyo ilikosolewa na China ambayo inamtazama kiongozi huyo kama anayejaribu kuitenganisha Taiwan na China. China inaiona Taiwan kama ni sehemu ya eneo lake.