1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yatoa filamu ya maandalizi ya jeshi kuivamia Taiwan

6 Agosti 2023

China imetoa filamu mpya kuhusu maandalizi ya jeshi ya kuivamia Taiwan. Filamu hiyo inawaonesha wanajeshi wakiahidi kujitolea uhai wao ikiwa watahitajika kufanya hivyo

Taiwan I Kampfjets der chinesischen Luftwaffe fliegen in Formation während eines Trainings am Stadtrand von Peking
Picha: Jason Lee/REUTERS

China imetoa filamu mpya kuhusu maandalizi ya jeshi ya kuivamia Taiwan. Filamu hiyo inawaonesha wanajeshi wakiahidi kujitolea uhai wao ikiwa watahitajika kufanya hivyo, wakati Beijing ikiendelea kujiimarisha dhidi ya kisiwa hicho kinachojitawala.

Soma pia: China yaituhumu Marekani kuigeuza Taiwan kuwa eneo hatari

Filamu yenye jina "Chasing Dreams" ambayo ni mfululizo wa sehemu nane ilirushwa hewani na televisheni ya taifa ya CCTV mapema wiki hii wakati wa maadhimisho ya miaka 96 ya jeshi la ukombozi la China.

Sehemu ya makala hiyo ilionesha mazoezi ya kijeshi na ushuhuda wa wanajeshi ambao baadhi yao walielezea utayari wao wa kufa ikiwa kutakuwa na shambulio dhidi ya Taiwan. China inadai kuwa, Kisiwa kinachojitawala cha Taiwan ni sehemu ya himaya yake na itatumia nguvu kukiweka chini yake kama italazimika kufanya hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW