China yawashauri raia wake kutosafiri Japan
15 Novemba 2025
Kyodo pia imeripoti kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Japan Minoru Kihara amesema nchi hiyo ilifikisha ujumbe kwa China na kuiomba ichukue hatua zinazofaa lakini haikunukuu ufafanuzi wake kuhusu hatua hizo.
Mvutano kati ya China na Japan wachochewa na tamko la waziri mkuu kuhusu Taiwan
Hapo jana, China iliwaonya raia wake dhidi ya kusafiri kuelekea Japan katika mzozo huo uliosababishwa na maoni ya Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi ambaye wiki iliyopita alisema kuwa shambulizi la China dhidi ya Taiwan linaweza kuzuwa hali ya kutishia maisha ambayo inaweza kusababisha majibu ya kijeshi kutoka Tokyo.
Kihara amesema Japan na China zinatofautiana katika suala hilo na ni muhimu kudumisha mawasiliano.
Kulingana na chombo cha habari cha serikali China News Service, mashirika matatu ya ndege ya China yamesema leo kwamba tikiti za kwenda Japan zinaweza kufutwa ama kubadilishwa bila malipo.