1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

China yawashinikiza wabunge kutoka nchi 6 dhidi ya Taiwan

28 Julai 2024

Wanadiplomasia wa China wanawashinikiza wabunge kutoka nchi sita kutohudhuria mkutano wa kilele unaoilenga China, utakaofanyika katika kisiwa kinachojitawala cha Taiwan.

Rais wa China Xi Jinping akizungumza wakati wa dhifa ya chakula cha jioni katika kasri la Elysee mjini Paris, Ufaransa mnamo Mei 6, 2024
Rais wa China Xi JinpingPicha: Ludovic Marin/AP Photo/picture alliance

Wanasiasa kutoka Bolivia, Colombia, Slovakia, Macedonia Kaskazini, Bosnia na Herzegovina, na nchi nyingine moja kutoka Asia ambayo haikutaka kutambulishwa, wamesema wamekuwa wakipokea ujumbe, simu na maombi ya dharura kwa mikutano ambayo ingekinzana na mipango yao ya kusafiri kuelekea Taiwan, kwa kile wanachoelezea kuwa ni juhudi za kukitenga kisiwa hicho kinachojitawala.

Mkutano wa Taiwan ni wa Muungano wa Mabunge kuhusu China

Mkutano huo unaanza kesho Jumatatu na unafanywa na Muungano wa Mabunge kuhusu China, kundi la mamia ya wabunge kutoka nchi 35 wanaojihusisha na jinsi mataifa ya kidemokrasia yanavyoshirikiana na China.

Taiwan ina uhusiano usio rasmi na nchi nyingi

Mara kwa mara China imekuwa ikitishia kulipiza kisasi dhidi ya wanasiasa na nchi zinazoonyesha kuiunga mkono Taiwan, ambayo ina uhusiano usio rasmi na nchi nyingi kutokana na shinikizo la kidiplomasia laChina.