China yazungumza na Myanmar kuhusu usalama wa mipaka
31 Oktoba 2023Hii inatokana na makabiliano kati ya makundi ya wapiganaji na jeshi nchini Myanmar.
Wang Xiaohong, ambaye pia ni mjumbe wa baraza la mawaziri la China linalofahamika kama Baraza la Taifa, alikutana na waziri wa mambo ya ndani wa utawala wa kijeshi wa Myanmar, Luteni Jenerali Yar Pyae, katika mji mkuu wa Myanmar, Naypyidaw.
Soma zaidi: Kambi ya wakimbizi Myanmar yashambuliwa kwa kombora
Maelfu ya watu wameripotiwa kuyahama makaazi yao, huku baadhi wakiingia China, baada ya makundi matatu yenye silaha yanayopigania uhuru kuanzisha mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya utawala wa kijeshi, ambao ulisema umepoteza udhibiti wa vituo kadhaa.
Makundi hayo matatu -- ambayo wachambuzi wanasema yanaweza kuwakusanya wapiganaji 15,000 kati yao, yamepigana mara kwa mara na jeshi kudai uhuru na udhibiti wa raslimali.