Christian Wulff ateuliwa kugombea urais wa Ujerumani
4 Juni 2010Matangazo
Viongozi walioko madarakani wanalazimika kumteua rais mpya kabla ya mwisho wa mwezi. Wakati huo huo, muungano wa vyama tawala vya CDU-CSU na Waliberali wa FDP wamemteua, Christian Wulff kugombea urais wa nchi. Christian Wulf aliye na umri wa miaka 50 ni kiongozi wa Jimbo la Lower Saxony, makao ya kiwanda cha kutengeneza magari cha Volkswagen.
Kwa upande wao vyama vya upinzani vinamuunga mkono Joachim Gauck, mwanaharakati wa kutetea haki za kiraia wa zamani na Mkurugenzi wa Shirika la kuhifadhi kumbukumbu za majasusi wa zamani wa Ujerumani, Stasi. Je hali hii inaashiria kipi? Nimezungumza na Abdallah Salim Mzee mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mkazi wa mji wa Potsdam ulio karibu na mji wa Berlin.