1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chuki dhidi ya wageni mashariki mwa Ujerumani zatia fora

23 Mei 2006

Hotuba kali ya rais Köhler WA Ujerumani mbele ya mkutano mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi la Ujerumani (DGB),visa vinavyozidi vya matumizi ya nguvu vya wafuasi wenye siasa kali wa mrengo wa kulia, ndio mada kuu zilizo chambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Gazeti la Kölnische Rundschau linatuanzia ukaguzi huu kwa mada ya wimbi linalozidi la visa vya wafuasi wenye siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani:

Laandika:

„Wajerumani wa asili na ran gi nyengine kwa bahati mbaya wanabidi kuchunga maisha yao humu nchini.Wanabidi kuyakimbia baadhio ya maneo huko mashariki mwa Ujerumani.

Hii ni hali ilioselelea tangu miaka mingi,lakini mara nyingi haipigiwi debe kama ilivyo sasa.Hata hivi sasa si idadi ya kutisha ya visa hivyo inayotufunua macho,bali ni matukeo fulani fulani tu.Alao jambo moja limekoma kusemwa:kwamba hivi ni visa vya hapa na pale tu.Labda huo unaweza kuwa mwanzo mwema.

Ama gazeti la Süddeutsche Zeitung likiendeleza mada hii lasema kuwa, msemaji wa zamani wa serikali Uwe-Karsten Heye alibidi kusema kimsingi ni ukweli wa hali ya mambo.Kuwa, hatari inayo mkabili yeyote asieonesha sura ya mjerumani kuhujumiwa huko mkoani Brandenburg, mashariki mwa Ujerumanini kubwa zaidi kuliko magharibi mwa ujerumani.

Itikadi kali za mrengo wsa kulia huko zimekuwa tatizo ambalo muda mrefu sasa limefumbiwa macho na halikutatuliwa vilivyo.Kwahivyo,wakati umewadia kulielewa barabara tatizo hilo:yaani vijana wengi katika mikoa ya mashariki mwa Ujerumani, wameambukizwa chuki za ukabila.Ukweli huu, lanasihi gazeti, haufai tena kudharauliwa.

Hata gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG lazungumza vivyo hivyo likiandika kutoka Mainz :shina la wanazi-mambo-leo kama zamani lipo mashariki mwa Ujerumani ambako unazi wa siku za nyuma haukujadiliwa barabara na kupanguswa kabisa vichwani mwa watu.

Kwa kutumia polisi zaidi,huwezi kufumbua kitandawili hiki,lasema Allgemeien Zeitung,kwani ufungo wake uko mashuleni na majumbani kwa wazee wa vijana hao.

Demokrasia mtu aweza kujifunza na kutoa historia ya Ujerumani ,kuna darasa la kujifunza athjari zake.Idadi ya visa, gazeti la hetimisha,yaonesha kazi kubwa ya kupiga vita chuki za kikabila, bado haikumalizwa.

Likitugeuzia mada, gazeti la NEUE OSNERBRÜCKE ZEITUNG linagusia hotuba kali alioitoa rais Köhler wa Ujerumani mbele ya mkutano mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi la Ujerumani-DGB.Laandika:

„Horst Köhler kimsingi hajakosea:Mapato zaidi ya kodi kwanza yapunguze gharama za ujira wa watumishi na kwa kufanya hivyo, yaruhusu kuongezeka kwa nafasi za kazi.Bila shaka, rais wa Ujerumani, alifika kikomo chake cha mwisho katika aliyosema mbele ya mkutano huu wa DGB.

Kwa vyama-tawala vya CDU na SPD maana ya yale aliotamkani kumtuliza shetani.Heba kuu ya hadhi ya rais isichafuliwe kwa ila za kumkosoa zisizostahiki.“-hayo ni maoni ya NEUE OSNERBRÜCKER ZEITUNG.

Gazeti la CHEMNITZER FREIE PRESSE limegundua katika hotuba ya rais mshikamano ulio nanda kabisa kati ya pande hizi mbili:

„Wajumbe wa vyama vya wafanyikazi na rais wa dola mhafidhina wameonesha kukaribiana zaidi kuliko ilivyodhaniwa kabla.

Na huu ndio msangao pekee kuhutubia mara ya kwanza rais wa Ujerumani ukumbi wa mkutano wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi.

Serikali ya muungano wa vyama viku,ndio uliowezesha hayo.“ -Chemnitzer FREIE PRESSE.

Likifuata nyayo za uchambuzi wa Kölnerstadt Anzeiger, gazeti la MÄRKISCHE ALLGEMEINE kutoka Potsdam laandika:

„Ila juu ya mpango wa utozaji kodi wa serikali zilitolewa vya kutosha.Na hii imedhihirisha kuwa serikali ya muungano ya vyama viku Ujerumani haitaki kuachana na mkondo huo potofu iliofuata.Kelele alizopiga na kuhanikiza rais wa Ujerumani ,ni vishindo vya darini,vilivyoishia sakafuni-havikubadili kitu“.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW